Mtoto mchanga aliyekadiliwa kuwa na miezi mitano amekutwa metupwa katikati ya Barabara katika kitongoji cha kinoni kijiji Nyabwegira kata ya ndama Wilayni karagwe.
Kichanga hicho ambacho kimekutwa kimekufa, kwa mujibu wa mashuhuda wameeleza kuwa kilionekana majira ya asubuhi ya jumapili 16june mwaka huu.
Jeshi la polisi wilayani karagwe wakiongozwa na OCS Edward Masunga pamoja na mganaga kutoka kituo cha Afya kayanga John Makonga wamefika eneo la tukio ambapo baada ya uchunguzi na taratibu zote kufanyika wameamuru mwili wa mtoto huyo kuzizwa eneo hilo.
Hata hivyo mganga makonga akiwa eneo la tukio baada ya uchunguzi na kuhojiwa na vyombo vya habari kama mimba imetolewa amesema kuwa imetoka bahati mbaya na kuwa kichanga hicho kilikuwa jinsia ya kike.
Pamoja na kuwa mwili wa mtoto huyo ulikutwa hatua chache karibu na makazi ya watu lakini wananchi walizungumza na waandishi wa habari wamesema kuwa hakuna mtu katika kitongoji na kijiji hicho aliyekuwa na mimba.
Wananchi hao wameeleza kuwa huenda aliyefanya kitendo hicho ametokea vijiji na vitongoji jirani.
Wamezungumzia kitendo hicho kuwa cha kinyama na kutaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali kwa atakayebainika kuhusika na tukio hilo.
kwa upande wa Jeshi la polisi Wilayani Karagwe wameomba wananchi pamoja na Vituo vya Afya ,zahanati na Hospitali Mkoanini Kagera kushirikiana na Jeshi hilo katika uchunguzi wa kumbaini aliyehusika na tukio hilo
Mpaka naripoti taarifa hii hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.
Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera Philip Karangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea
No comments:
Post a Comment