Hilo ni jina la mbunifu mmoja Ezekiah Kyakatuka mkulima aliyebuni dawa ya kutibu ugonjwa wa mnyauko unaotishia kutowesha zao la ndizi mlezi na kipenzi cha wahaya mkoani kagera.
Dawa hiyo haijathibitishwa na watalaam lakini imeelezwa kuwa na mchanganyiko wa aina nane {8} za miti shamba.
Hii inaonesha ni namna gani Wakulima wa zao la ndizi mkoani kagera wana machungu na kutoweka kwa zao hilo hivyo kuamua kulivalia njuga
suala la ugonjwa fudhari{ Mnyauko} unaoshambulia migomba.
Ezekiah Kyakatuka ni mkulima mkazi mtaa wa Nsheshe kata ya kayanga wilayani Karagwe ambaye amebuni dawa ya unonjwa huo lakini haijathibitishwa na wataalam.
Akihojiana na mwandishi wa habari ametaja dawa hiyo kuwa
binafsi ameita jina la "Njuna wejune Embwa yatwala ekirumiko" likiwa na maana ya kuwa leo kwako kesho kwangu, yenye mchanganyiko wa aina nane {8} za dawa ya miti shamba.
Aina hizo ni:
1.Mkojo kiasi cha ujazo wa ndoo au diaba
2.Majivu
3. Majani ya mti wa Mruku
4.Majani ya tumbaku
5.Majani ya mti wa Kajae
6.Majani ya mti wa Omumemenwa
7.Majani ya mti wa Jutrofer {kakalakare}
8.Mti wa Enkukuru
Maelezo ya dawa hizo anasema vuna majani ya kutosha, changanya katika ndoo yenye mkojo, kata tawi katika vipande vipande alafu twanga.
Dawa yote iliyokusanywa changanya pamoja katika ndoo au kwenye diaba yenye mkojo na majivu kisha anza kuitumia baada ya siku mbili au tatu pia funika isijeingia maji ya mvua.
MATUMIZI:
Hutumika kwenye mgomba wenye ugonjwa katika kisiki{ Ekikuzi} chimba shimo kwenye kisiki cha mgomba uliokatwa chukua dawa kwenye kopo mwaga kwenye kisiki na ufunike na majani ya migomba{Embabi}, kama kisiki hicho kina machipukizi mengi punguza ubakize chipukizi moja au mawili pia uangalie kukua kwa chipukizi hilo.
Anasema kuwa Dawa hiyo ikikaa kwenye ndoo kwa muda mrefu haiharibiki unaweza kuitumia mpaka pale itakapo kwisha na kutafuta nyingine.
Je ye ameishawahi tumia dawa hiyo? Na kama ametumia
amepata mafanikio au faida gani?...........anasema yeye ametumia dawa hiyo kwa kipindi cha mwaka mzima 2012 na matokeo yake migomba yake imestawi vizuri.
Mwandishi wa habari hii amehoji juu ya upatikanaji wa kiasi cha mkojo alichotaja na kujibu kuwa "mtu akiona faida yake anaweza pata hata shuleni"
Mzee Kyakatuka anawashauri wakulima wa mkoa wa kagera kujaribisha ubunifu huo kuona kama watakomboa kutoweka kwa zao la ndizi mkoani humo.
Kwa maelezo yake Mzee Kyakatuka, dawa hii haijathibitishwa na
wataalam lakini amesema kuwa amepeleka nakala kwa mkurugenzi mtendaji wa
halmashauri ya wilaya ya karagwe na kuahidi kulifanyia kazi suala hilo.
Itakumbukwa kuwa wakulima wa zao hilo mkoani kagera
sasa ni kilio kupoteza zao hilo kutokana na ugonjwa huo.
Wakulima wa zao hilo mnasemaje, tunajua mbinu nyingi zimetolewa kuhakikisha ugonjwa huu unaisha lakini mafanikio yake bado ni hafifu.
Nani atauondoa na kwa njia zipi?
No comments:
Post a Comment