WANAWAKE WAJANE WILAYA YA KARAGWE NA KYERWA {UWK} KUZURU
KABURI LA BABA WA TAIFA HAYATI MWL JULIUS KAMBARAGE NYERERE, BUTIHAMA MWITONGO SEPTEMBER
2013.
Umoja wa wanawake wajane na yatima wilayani Karagwe na
Kyerwa wameandaa ziara ya kwenda
kutembelea kaburi ya baba wa taifa hayani Mwl Julius K.Nyerere kiwa ni pamoja
na kumtembelea mama Maria Nyerere ka majane pia buga za Wanyama SERENGETI.
Lengo la ziara hiyo ni wanawake hao kubadilishana mawazo na mjane mwenzao na mama Maria Nyerere.
Akitoa ufafanuzi wa ziara hiyo mwenyekiti wa UWK Bi Grace
Mahumbuka amesema imetokana na azimio la kamati tendaji ya Umoja huo 23 June
2012 katika kikao cha kwanza baada ya uchaguzi mkuu wa viongozi uliofanyika 27
April 2012 kilichoazimia kufanya hija ya kuzuru kaburi la Baba wa taifa.
Vile vile wataunganisha safari ya kwenda kutembelea mbuga za
wanayama SERENGETI kwa madhumuni ya kuhamasisha utalii wa ndani katika makundi
na kwa mtu moja mmoja nchini Tanzania.
Ziara hii pamoja na maandalizi inaongozwa na mkuu wa mkoa wa
kagera Cal Fabian Inyasi Massawe, Mkuu wa wilaya ya Karagwe Bi Dary Lwegasira
na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Cal Benedicto Kitenga.
Bi Mahumbuka amewaeleza waaandishi wa habari kuwa kamati
tendaji ya UWK kwa niaba ya mkutano mkuu
wa UWK ilisha mwandikia barua mkuu wa mkoa Cal Fabian Massawe yenye kumbukumbu No.UWK/KRD/VOL.7/07/2012
ya tarehe 19October 2012 na nakala kwa wakuu wa wilaya mbili Karagwe na Kyerwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya
wilaya ya Karagwe kwa ajili ya maadalizi mapema.
Wanawaka hawa wajane wataambatana na burudani za Tamaduni
wakiwemo watu wa majigambo ya Lugha ya Kinyambo, vikundi vya Ngoma kutoka
Chanika Karagwe, Maigizo na Nyimbo za
hamasa kutoka kwa wanawake wajane.
Gharama kwa waotaka kushiriki ziara hiyo hususani wanawake
ni shilingi 120,000/= kwa kila mtu kwenda na kurudi.
No comments:
Post a Comment