WAZEE WAMEKUWA KITEGA UCHUMI KWA WENYE UWEZO.
Inakumbukwa mnamo tarehe mosi October 2010, waziri wa
Jamuhuri ya Muungano Wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda kupitia hotuba
yake katika mahadhimisho ya siku ya wazee duniani aliseme matibabu bure kwa
wazee halina mjadala.
Alisema hayo katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Tangu kutolewa kwa tamko hilo mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali yamelivalia njuga na kuunganika na mashirika yanayohudumia wazee
nchini ili kuunganisha nguvu na sauti za pamoja za wazee kudai haki na stahiki
zao.
Pamoja na juhudi za mashirika hayo yapo mashirika bandia
yaliyoibuka kupitia migongo ya mashirika hayo kuwarubuni wazee kuchangia fedha ambazo hazikuwa na viwango maalum wakidai kuwapatia huduma ya Afya bure,
pensheni na huduma nyingine zinazodaiwa na wazee kutoka serikali ya Tanzania.
Hata hivyo matatizo ya wazee yamebaki pale pale kwani waliochukua fedha za
wazee hao na kuwaorodhesha hawakurudi tena.
Kutokana na vitendo hivyo kuripotiwa kujitokeza sehemu
mbalimbali hapa mkoani Kagera shirika la SAIDIA WAZEE KARAGWE {SAWAKA} kupitia kwa mwenyekiti wake Mzee Nekemia
Kazimoto LIMETOA RASMI TAMKO KWA MASHIRIKA HAYO HEWA kuwa haliyatambui mashirika hayo.
Taarifa hiyo kwa vyombo vya habarri imeeleza kuwa shirika la SAWAKA limepokea malalamiko toka
kwa wazee katika sehemu mabalimbali za wilaya ya Karagwe na Kyerwa,
wakilalamikia kuwa wamerubuniwa na baadhi ya watu toka shirika lisilojulikana
ambalo limeanza hivi karibuni kwa kuwatoza wazee shs 2,500/= kwa kuwapatia
vitambulisho vya kuwatambulisha wazee kwa ajili ya matibabu na huduma
mbalimbali bure toka serikalini.
Na kwamaba wazee hawa wamekuwa wakivipeleka
vitambulisho hivyo katika vituo vya Afya na Hospitali kama vile Nyakahanga na
kufukuzwa kwani havina uhalali na havikutolewa na mamlaka husika.
Hivyo wazee na jamii inayowahudumia imewekwa wazi kuwa Vitambulisho
vya wazee vinavyotolewa na shirika hilo havina uhalali wowote kwani havina
baraka za serikali na havitambuliwi na mamlaka husika na havina anuani wala
muhuri wa wahusika kuthibitisha uhalali wake.
Shirika la SAWAKA linawaakikishia wananchi woto karagwe na Kyerwa kwamba haina uhusiano wala ushirikiano
wowote na kundi hilo au shirika husika.
Katika ufuatiliaji wake wamebaini kuwa hakuna shirika au Asasi iliyo hai
ijulikanayo kama῝wazee wa Taifa la
Tanzania῞ ambayo imepewa jukumu la kutoa vitambulisho hapa nchini na kuongeza kuwa kama lipo ndizo zile Asasi za
mfukoni ambazo zinatia doa shughuli za kazi nzuri za NGO’s.
Kwa tamko hilo Wazee wanatahadharishwa kutochukua
vitambulisho hivyo kwani vinatia mashaka sana na kuwataka viongozi wa matawi ya
SAWAKA yaliyopo vijijini kuwaelimisha wazee kuwa na subira ya kupata
vitambulisho vya mapema mwaka huu kama serikali ilivyokwisha toa ahadi.
Taarifa hiyo imesema kuwa Vitambulisho hivyo bandia kwa
wazee vimeanza kutolewa katika wilaya za Karagwe hasa Nyakahanga, Kihanga,
Chanika, Nyaishozi, na Ihembe,ambapo wasi wasi mkubwa ni kwamba huenda kundi hilo likaendeleza mchezo huu katika
wilaya jirani za Muleba, Misenyi na
Bukoba.
Wayaomba mashirika
ambao ni washirika wao wanayofanya nayo
kazi kma TUWAMI, NA KWA WAZEE kuwaelimisha wazee kuhusu utapeli huu ambao
unaonekana kuwa mradi wa watu wachache wanaotafuta kujinufaisha na fedha za
wazee.
SAWAKA kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Karagwe
na Kyerwa, imewomba wazee kuvuta subira kuwa watatioa taarifa juu ya utaratibu
utakaotumika pindi serikali itakapokamilisha mchakato huo.
Suala hili limefikishwa serikalini na kuthibitisha kuwa vitambulisho hivyo ni
bandia na kutoa taarifa kwa vyombo husika ili wahusika wakamatwe na kuchukuliwa hatua za sheria huku wazee wakiombwa kutoa ushirikiano wa kuwabaini wanaotoa
vitambulisho hivyo bandia kwa wazee.
No comments:
Post a Comment