Friday, January 18, 2013
NANI ACHOCHEE UTEKELEZAJI WA HUDUMA YA MATIBABU BURE KWA WAZEE?
NANI ACHOCHEE UTEKELEZAJI WA HUDUMA YA MATIBABU BURE KWA WAZEE?
Na
Adelina Nestory
Karagwe
WAZEE wilayani Kyerwa wameiomba serikali kuboresha huduma ya afya ili kukithi haja ya mahitaji yao.
Wakizungumza na waandishi wa habari badhi ya wazee hao ambao wamesema kuwa wamekuwa wakitaabika kupata huduma ya afya na kulazimika kuingia gharama kubwa hivyo kukata tamaa ya matibabu hospitalini badala yake wanatumia mitishamba lakini bila mafanikio.
Serikali kupitia kwa waziri mkuu wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda iliagiza wazee wote kupata huduma ya matibabu bure,agizo alilolitoa katika hotuba yake 1october 2010 mkoani morogoro wakati wa mahadhimisho ya siku ya wazee duniani.
Lakini utekelezaji wake ni hafifu wazee wanalalamika, kwa nini agizo hilo limetupiliwa mbali.
Na
Adelina Nestory
Karagwe
WAZEE wamejiwekea mikakati ya kupigania haki zao katika kupata huduma za msingi kama huduma ya afya bure kama inavyo tamkwa, pensheni kwa wazee wote na sera ya wazee kutungiwa sheria.
Wazee hao ni wale wajumbe wawakilishi wa wazee kutoka katika kata mbalimbali za wilaya ya karagwe na kyerwa wamejipanga kunganisha sauti za pamoja kudai haki zao katika vyombo vinavyotoa maamuzi.
Kubwa zaidi walilolitamka kwenda kufanya ni kutoa maoni yao juu ya masuala yanayowahusu wazee kuingizwa katika katiba mpya inayokwenda kuandikwa.
Suala la makundi yanayojifanya mashirika ya kusaidia wazee kwa kuvaa kivuli cha mashirika yanayofanya kazi hiyo linazidi kujitokeza maeneo mbalimbali ya vijijini wilayani karagwe na kwingineko mkoani kagera.
Hali hii inawafanya wazee kushindwa kutambua lipi shirika linalofanya kazi ya kuhudumia wazee bila michango isiyo ya lazima na msingi.
Makundi haya yameelezwa kupitia mgongo wa washirika yanayotambulika kuhudumia wazee na kuchangisha pesa isiyokuwa na viwango.
Kigezo wanachokitumia kuwadanganya wazee ni kuwa watawaletea pensheni, matibabu bure pamoja na huduma nyinginezo za msingi zinazodaiwa na wazee.
Hata hivyo tahadhari imetolewa kwa wazee pamoja na jamii inayohudumia wazee kuwa makini na watu hao na kuwa endapo wana nia ya kuwasaidia wasimamie malengo yao si migongo au vivuli vya watu wengine bila idhini ya kufanya hivyo.
Inakumbukwa mnamo 9 November mratibu wa shiria la saidia wazee Karagwe SAWAKA Bw Livingistone Byekwaso kwa kuwa shirika hilo ndilo linalotumiwa na makundi mengine kama kivuli chao, ametoa ufafanuzi juu ya upatikanaji wa pensheni na matibabu bure kwa wazee kuwa wasikubali kuddanganyika kuwa yupo mtu anayeweza kutoa pensheni na matibabu bure bila kufuata utaratibu.
Amesema wanaofanya hivyo ni mataperi lazima wawaepuke mara moja na kutoa taarifa kwa shirika hilo.
Na
Adelina Nestory
Karagwe
JAMII inayoishi na wazee imeombwa kuwasaidia kwa kuwaelimisha kuwa makini na udanganyifu unaoendelea kujitokeza katika maeneo mbalimbali kuwa hakuna huduma ya afya bure na penshini inayotolewa na mtu yeyote zaidi ya serikali.
Wakati huo huo kusahaulika kwa wazee katika kupata huduma muhimu na za msingi si kigezo cha kuwakatisha tamaa ya kutoendelea kudai stahiki zao.
Wakizungumza na fadeco redio kwa nyakati tofauti wamesema kuwa jamii na serikali wakae na kufikiri kuwa kuna kundi la wazee pia kutambua umuhimu na mchango wao katika maendeleo ya taifa.
Wamekieleza chombo hiki namna pensheni kwa wazee wote itakavyo wasaidia na wengine wakiwa na shahuku ya kuwaona viongozi ana kwa ana kutoa matakwa yao.
Na
Adelina Nestory
Karagwe
WATOTO 524 wanaoishi katika mazingira hatarishi wilayani ya karagwe na kyerwa wamepata vyeti vya kuzaliwa kutoka katika ofisi ya usajiri vizazi na vifo iliyopo wilayani hapa.
Akithibitisha kutolewa kwa vyeti hivyo mratibu wa shirika la saidia wazee karagwe bw Livingstone Byekwaso amesema kuwa pamoja na kusaidia wazee wanawasaidia pia wategemezi wao ambao ni watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi.
Ametaja kazi inayofanya na shirika hilo katika mradi wa kusaidia watoto kuwa ni kutetea haki zao ambapo ameongeza kuwa wamebaini watoto wanaoishi katika mazingira magumu hawana vyeti vya kuzaliwa kutokana na wazazi na walezi wao kutokuwa na uwezo.
Kwa upande wake mmoja wa wazazi wa watoto hao waliopata vyeti akihojiana na fadeco redio ameonesha kufurahishwa na msaada huo kwani ameeleza uwezo wake mdogo asingefanikiwa kukipata ambapo watoto 20 katika kata ya bugene wamepata vyeti wakiwemo wakwake wawili.
Mafanikio mengine yaliyopataikana kututoka katika shirika la SAWAKA wakishirikiana na Help Age Internation pamaoaja na mashirika mengine wamewaunganisha wazee kuwa kitu kimoja ili kurahisisha upatikanaji wa huduma zao za msingi.
Na
Adelina Nestory
Karagwe
SHIRIKA la kusahidia wazee wilayani karagwe [ SAWAKA] limeiomba serikal kutoa
Mafao ya uzeen na huduma za kijamii kwa wazee ili kuwaondoa katika mazingira Hatarishi.
Ombi hilo limetolewa na mratibu wa SAWAA bw Livingston Byekwaso katika warsha
Ya kujadili mambo mbalimbali ya kuwasaidia wazee iliyofanyikia wilayani muleba kwa udhamini wa shirika hilo.
Warsha hiyo iliyoudhuliwa na viongozi mbalimbali wa wilaya hiyo;mkurugenzi pamoja
Na viongozi hao wamesema wazee wamekuwa wakiishi kwa shida hivyo ni vyema serikali ikawaangalia kwa jicho la pili.
Aidha changamoto mbalimbali zinazowakabili wazee ni pamoja na kutokuwa na huduma bora ya afya,kufanyiwa vitendo vya ukatiri hasa kuaribiwa mali zao na wakati mwingine
Kuuwa.
Pia wamekuwa hawapati matibabu stairi ya afya zao pamoja kutopewa mafao ya uzeeni
Hivyo kusababisha uduni wa maisha kwa wazee hao hapa nchini.
Shirika la SAWAKA limetoa misahada mbalimbali ya kuwainua wazee
Kiuchumi kuelimisha jamii juu ya kuwathamini wazee hivyo limeomba ushikiano
Kutoka kwa serikali na wananchi kwa ujumla .
Nao washiriki wa warsha hiyo wameaidi kutoa mchango mkubwa hasa kuelimisha jamii umuhimu wa wazee pamoja na kutoa maoni yao ya kuundwa kwa sheria ya kuwalinda wazee katika uhundwji wa katiba mpya .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment