ELIMU KIPAUMBELE CHA KWANZA MWAKA 2013 MKOANI KAGERA.
Wazazi na walezi wametakiwa kuwapeleka
watoto wao shule waliochaguliwa kujiunga na masomo ya sekondari ndani ya wiki moja.
Kauli hii imetolewa
na mkuu wa mkoa wa Kagera Cal Fabiani .I. Massawe katika ziara yake ya kagua
miradi ya maendeleo wilayani Karagwe mkoani humo baada ya mkuu wa shule ya sekondari ya Ndama
kusoma taarifa iliyobainisha
mapungufu ya wanafunzi 200 waliochaguliwa kujiunga na shule
hiyo ni wanafunzi 40 tu waliripoti kuanza masomo ya sekondary.
“ Nimesikiliza taarifa ya shule lakini bado,Wazazi
wote na walezi ambao hawajapeleka watoto walifaulu kuanza kidato cha kwanza
nawapa wiki moja kuhakikisha watoto hao wanakwenda shule na viongozi mfuatilie”
Cal masawe amesema kufanya hivyo itasaidi kupiga
hatua ya maendeleo kielimu kwani ndicho kipaumbele cha kwanza kwa mwaka 2013
kati ya miradi mingine ya maendeleo mkoani Kagera.
Wakati huo amewataka Watendaji wa halmashauri wa wilaya za Karagwe na Kyerwa kusimamia vema
miradi ya maendeleo na kuwa waadilifu na uwajibikaji wa miradi ya maendeleo na serikali iliyopo
madarakani kwa ajili ya kuwahudumia wananchi wake.
Amesema kuwa endapo viongozi watasimamia vema miradi ya maendeleo na kuongoza wananchi kwa uadilifu
ufanisi katika shughuli za maendeleo seikali iliyo madarakani
itatimiza malengo yake ya
kuwahudumia wananchi wa kada zote na kuondoa manunguniko yaliyopo kwa sasa.
Katika ziara hiyo mkuu wa Mkoa ametembelea miradi
mbalimbali ya maendeleo ikiwemo mradi wa
ujenzi wa chuo cha ualimu Karagwe
kilichopo kata ya Ihanda,mradi wa umwagiliaji wa Mwisa Bujuruga,mradi wa maji
wa Charuhanga, kukagua ujenzi wa bweni la wasichana Shule ya sekondari ya
Kiruruma ,ujenzi wa Zahanati ya
Omurusimbi na kukagua miradi mbalimbali ya shirika la MAVUNO yote ya wilayani humo.
No comments:
Post a Comment