Thursday, January 24, 2013

“BUSARA NA MOYO WA HURUMA VINAHITAJIKA KUWAHUDUMIA WATU WENYE ULEMAVU”



            “BUSARA NA MOYO WA HURUMA VINAHITAJIKA KUWAHUDUMIA  WATU     WENYE ULEMAVU”               
                                       

                                 
                                               
                            Bi Meduled Yohana {37}  mlemavu wa miguu anayelea familia ya watoto 8 yatima.



Watu wenye ulemavu wa aina mbalimbali wanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kubeba majukumu ya kutunza familia, kunyanyapaliwa na uwezo mdogo kiuchumi.


Hali hii imewafanya kukata tamaa ya maisha hasa pale wanapokosa msaada wa majukumu kama kusomesha watoto, chakula na malazi pia mitaji ya kuendesha shughuli ndogo ndogo za uzalishaji wazojishughulisha nazo.


Bi Meduled Yohana mkazi wa kata ya kibingo wilaya ya Kyerwa Mkoani Kagera mwenye umri wa mika {37}  ni mmoja wa watu wenye ulemavu wa miguu yote miwili na analea watoto wanane {8} yatima.



Ulemavu wake ni wakuzaliwa nao, ana mtoto mmmoja {1]  umri miaka {8} darasa la kwanza katika shule ya msingi Kibingo wilayni humo ambapo mme wake amefariki mwaka 2001.
Akihojiana na mwandishi wa habari hii ameeleza tatizo linalomsumbua kuwa ni gharama za masomo na  mahitaji mengine ya msingi kutunza familia.


Bi Yohana anasomesha watoto saba  {7} katika shule ya msingi KIBINGO  wawili{2}  wakiwa darasa la saba ,mmoja {1} darasa la nne {4}, mmoja {1} darasa la tano, wawili {2} darasa la tatu{3}  na mmoja {1} darasa la kwanza {1}  Na amepokea barua kutoka kwa mwalimu mkuu wa shule hiyo iliyobainisha mahitaji ya shule kama una mwanafunzi shuleni hapo kama hapa ilivyo nakiriwa na mwandishi wetu:-
                                                                                                                                                                                
                                                                            S|M Kibingo
Box 102
Karagwe
22.01.2013
                                                                                                                                                                                                                                                                                                                 YAH:MAHITAJI YA WANFUNZI KWA MWAKA MZIMA 2O13.


Rejea kichwa cha barua hapo juu cha husika. 

Ninaomba kubainisha mahitaji ya wanafunzi kwa mwaka.Kwa wanafunzi wafuatao:

(1)kwa darasa la saba na darasa la nne

(a)sare ya shule (b)viatu na sokisi (C)Awe na daftari na kalamu (d)mfuko imara (e)michango ya shule kama ifuatavyo:

1 sh 3000x @ kwa ajiri ya malipo ya walimu wa ziada (kujitorea)na mlinzi.

(2)sh 4000 x2@kwa ajiri ya masomo ya ziada.

(3)sh 2000x2@ kwa ajiri ya kitabu cha taarifa ya maendeleo ya mtoto,hiki ni kwa kipindi chote cha masomo yake yaani darasa la 1-7

e) Ikiwezekana anunuliwe vitabu ambavyo vinaweza kuwa msada wa kujisomea.
(2)kwa wanafunzi tofauti na madarasa hayo mahitaji ni
(1)sh 3000x2@ walimu waziada na mlinzi.
(2)sh 2000x@ kitabu cha matokeo
Asanteni
Mwalimu mkuu
Shule ya msingi KIBINGO
KARANGWE


Hiyo ni barua iliyonakiriwa na mwandishi wa habari kutoka kwa mkuu wa shule ya msingi kibingo Na kupokelewa na mzazi pia mlezi  Bi Meduled Yohana  mwenye watoto saba  {7} katika shule hiyo wawili{2}  wakiwa darasa la saba ,mmoja {1} darasa la nne {4}, mmoja {1} darasa la tano, wawili {2} darasa la tatu{3}  na mmoja {1} darasa la kwanza {1} wote wakiwa yatima.barua hii  inabainisha mahitaji yanayohitajika.


Bi Meduled Yohana akionesha barua za madai ya gharama za masomo.


Vile vile Mama huyu anamsomesha kijana mmmoja Godfrey Edward katika shule ya sekondari IBANDA kidato cha tatu lakini matatizo ni yale yale gharama hakuna.


Karatasi ya pili imeonesha gharama anazodaiwa mwanafunzi huyo katika shule hiyo ya sekondary tangua aanze kidato cha kwanza mwaka 2011 hadi sasa 2013 na kufikia jumla ya shilingi 363,500/= kama ifuatavvyo:-



MADENI YA GODFREY EDWARD F I-II 2011-2013.
Deni mwaka 2011—153,500/=+85,500/=
        Mwaka 2012 – 85,500/=+62,000/=
        Mwaka 2013 --- 105,500/=
Mwaka 2011 – 153,500/=+52,000/=
Mwaka 2012 – 85,500/=+62,000/=
Mwaka 2013 – 105,500/=


Deni F.I Mwaka 2011 --- 135,500/=
Deni F.II Mwaka 2012 ---107,500/=
Deni F. III Mwaka 2013 --- 105,500/=
        Jumla =348,500/= + 15,00/=  za Tution.
       Jumla kuu =363,500/=.


Boarding + Tution
1.       75,000/= kwa muhula
2.       Gunia {1} la mahindi
3.       Maharage debe tatu {3}
4.       Sare ya kushindia, suruali Nyeusi na T.Shert ya Bluu
5.       Godolo moja {1}, Blanket, mashuka ya bluu na viatu.
Hivyo anaomba msaada wa gharama hizo.

 
Bi Meduled Yohana akiwa na mwenzake Bi Evodia Philipo{35} mlemavu wa mguu mmoja wakihojiwa na mwandishi wa habari kutoka kituo cha Fadeco Redio Karagwe-Kagera.


Bi Meduled Yohana amezaliwa katika familia ya watoto wanne{4} wasichana wawili{2} na wavulana wawili {2} ambao msichana na mvulana wameishafariki na wameacha watoto wanaolelewa na mama huyo, na kaka yao mmjona aliyebaki {Vedasto Yohana} ana matatizo ya tumbo baada ya kupata ajali hufanyiwa oparation kila mwaka pia uwezo wake mdogo.


Ana uwezo wa kushona nguo kwa kutumia mikono ambapo chelehani anayotumia kwa sasa ameazima kutumia  kwa muda.

No comments:

Post a Comment