Wafanyabiashara wilayani karagwe hususani wanaojihusisha na uuzaji wa vifaa vya ujenzi ikiwemo saruji na chokaa wamewaomba wateja wao kukubaliana na bei iliyopo ya vifaa hivyo kwani hubadilika kila wakati hii ni kutokana na mfumuko wa bei hapa nchini.
Wakizungumza na fadeco redio kwa nyakati tofauti wafanyabiashara hao wamesema bei ya saruji imeshuka ikilinganishwa na mwaka jana,huku wakitaja bei hizo kuwa
SARUJI aina ya simba imeshuka kutoka sh:22,000/= hadi sh:20,500/= Kwa wanunuzi wa jumla na sh:20,000/= kwa wale wa rejareja.
Kwa upande wa CHOKAA aina ya Rhino imepanda kutoka sh:14,500/= hadi Sh:15,000/= kwa bei ya rejareja.
Hata hivyo wafanyabiashara hao wabainisha baadhi ya changamoto wanazo kumbana nazo kuwa ni pamoja na bidhaa inapo panda na kushuka bei wanapata hasara kwani wanakuwa wamenunua bidhaa nyingi,pia mifuko kutoboka wakati wa kupakia na kupakua mizigo.
No comments:
Post a Comment