Friday, January 18, 2013

UHURU WA BENDERA WAJIDHIHIRISHA WAZI, USALAMA NA AMANI HAKUNA, VITA YA WENYE KWA WENYEWE MTINDO MMOJA.

UHURU WA BENDERA WAJIDHIHIRISHA WAZI, USALAMA NA AMANI HAKUNA, VITA YA WENYEWE KWA WENYEWE MTINDO MMOJA. Na Adelina Nestory Karagwe Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanal Fabian Inyasi Massawe anatarajia kuanza ziara ya kukagua miradi ya maendeleo wilayani Karagwe 21 january mwaka huu. Taarifa kutoka kwa katibu tawala wa wilaya hiyo Mstafa S. Said kwa vyombo vya habari imebainisha miradi itakayokaguliwa na mkuu wa mkoa huyo kuwa ni ujenzi wa maabara katika shule ya secondary Ndama, mradi wa umwagiliaji mwisa Bujuruga, mradi wa maji Charuhanga na ujenzi wa chuo cha ualimu Ihanda. Miradi mingine itakayotembelewa ni MAVUNO Chonnyonyo,Bweni la wasichana shule ya secondary Kiruruma, kituo cha walemavu Chabalisa na Ujenzi wa zahanati ya kijiji Omurusimbi. Ziara hii ya mkuu wa mkoa wa Kagera inalenga kuchochea uchangiaji wa miradi ya maendeleo ya wananchi wilayani Karagwe na Taifa kwa ujumla. Na Adelina Nestory Karagwe Maskari wametakiwa kujitambulisha katika uongozi wanapokwenda kufanya kazi yao ili watambulike katika sehemu husika kuepusha vurugu na mauaji. Rai hiyo imetolewa na katibu tawala wilaya ya Karagwe Bw Mstafa S. Said wakati akijibu maswali ya waanchi katika mkutano wa wa kijiji cha nyaishozi uliofanyika january 18 mwaka huu ukiwahusisha viongozi wa wilaya ya Karagwe. Kauli hiyo imekuja baada ya wannchi kuhoji juu ya lawama zinazorushwa kwa waannchi kuhusu mauaji ya maaskari wawili kutoka Wialaya ya Ngara yaliyotokea siku za hivi karaibuni mwezi huu katika kata ya Rugu wilayani humu. Bw Said amesema kuwa maaskari hao waliingia wilayani karagwe bila kutoa taarifa kwa uongozi wa kijiji hicho na pia walivaa kiraia hali iliyosababisha raia kushindwa kuwatambua askari na kukemea tabia hiyo ambapo amemwagiza mkuu wa polisi wa wilaya OCD kuliangalia upya suala hilo. Ameongeza kuwa hata skari upelelezi anapokwenda kufanya kazi ya upelelezi anatakiwa kujitambulishwa kwa uongozi anapokwenda kufanya kazi hiyo ili wamtambue. Sambamba na hayo amewataka wananchi kudumisha ulinzi shirikishi na pia kuhakikisha kila mmoja analinda usalama wa sehemu anakoishi na kuepuka tabia ya kujichukulia sheria mkononi.

1 comment: