SHIRIKA LA SAIDIA WAZEE KARAGWE {SAWAKA} LATOA TAMKO RASMI JUU YA WANAOTAKA KUWATAPELI
WAZEE.
TAMKO LA MATIBABU BURE KWA WAZEE LA ZUA TAFULANI.
Inakumbukwa mnamo tarehe mosi October 2010, waziri wa Jamuhuri
ya Muungano Wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda kupitia hotuba yake katika
mahadhimisho ya siku ya wazee duniani aliseme matibabu bure kwa wazee halina
mjadala.
Alisema hayo katika uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro.
Ndugu wananchi, Mkutano ule wa mwaka jana nilisema kwa upande wa vituo vya afya na
zahanati, wazee wapewe huduma ya matibatu bure.
Hili halina mjadala,
hakuna sababu ya kununa maana halikuhusu.
Sera imeamua, Mkuu wa Nchi amesema,
sisi tunalipigia kelele, wewe mpe dawa aondoke aende zake, wewe cha kufanya ni
kutoa taarifa kwa wakubwa zako nimemhudumia mzee fulani na kumpa dawa bure, wao
watajua la kuufanya.
Tusilifumbie macho!
Kazi yetu TAMISEMI ni kufuatilia na kuona suala linafanyika kikamilifu.
Safari hii nataka
niongezee kidogo. Nataka niombe Wizara ya Afya ione ni namna gani tunaweza kuwa
na utaratibu wa kupeleka waganga kutoka hospitali za wilaya na mikoa kwenda
kwenye maeneo ya vijijini na kupiga kambi kwa siku kadhaa ili kupima afya za
wazee na kuwapatia huduma hasa kwa yale magonjwa ambayo hayawezi kutibiwa na
waganga tulionao katika ngazi ya zahanati na kituo cha afya.
Kwa kuanzia, tukifika
angalau katika ngazi ya tarafa, itasaidia sana.
Tukumbuke wapo wazee wengi wasioweza
kumudu gharama kufika katika hospitali za wilaya na mikoa kupata matibabu
wanayostahili.
Ni bora tukatumia muda
na posho ya Halmashauri kidogo kwa jambo hili, hakuna atakayekulalamikia hata
kidogo.
Na huo utaratibu ukishaanzishwa sasa
uwe wa kudumu kila mwezi lazima mtaalamu aende kupiga kambi kwa siku tatu au
nne. Napenda niamini tunaweza.
Naomba Wizara ya Afya
na TAMISEMI mshirikiane, ili tuone jambo hili ndani ya muda mfupi ujao
linafanyika kwa mafanikio.
Hiyo ni sehemu
ya hotuba ya waziri Pinda october mosi 2010 wakati akiwahutubia wananchi mkoani
Morogoro siku ya wazee duniani.
Tangu kutolewa kwa tamko hilo mashirika yasiyokuwa ya
kiserikali yalilivalia njuga na kuunganika na mashirika yanayohudumia wazee
nchini ili kuunganisha nguvu na sauti za pamoja za wazee kudai haki na stahiki
zao.
Pamoja na juhudi za mashirika hayo yapo mashirika bandia
yaliyoibuka kupitia migongo ya mashirika hayo kuwarubuni wazee kuchangia fedha ambazo hazikuwa na viwango maalum wa
kidai kuwapatia huduma ya Afya bure, pensheni na huduma nyingine zinazodaiwa na
wazee kutoka serikali ya Tanzania.
Kama inavyoeleweka mzee kama mzee akili yake ni kama mtoto
mdogo kutokana na hali zao, umaskini na kukosa huduma za msingi katika
kuhimarisha maisha yao ya uzeeni, walibabaika wengine wakachangia, wengine
kutafuta kwa udi na uvumba na kuona mashirika yanayotambulika kama yalikuwa
hayafanyi kazi kuwatetea wazee sasa wakombozi wamepatikana.
Hata hivyo matatizo yakazaa matatizo kwa wazee hawa kwani
waliochukua fedha za wazee hao na kuwaorodhesha hawakurudi tena.
Ninakumbuka mkuu wa
wilaya ya Misenyi Mkoani Kagera Cal Issa Suleiman Njiku, amewahi kusikika katika
vyombo vya habari akitahadharisha hali hiyo baada ya kutokea wialayani humo.
Kutokana na vitendo hivyo kuripotiwa kujitokeza sehemu
mbalimbali hapa mkoani Kagera shirika la
SAIDIA WAZEE KARAGWE {SAWAKA} LIMETOA
RASMI TAMKO KWA MASHIRIKA HAYO HEWA KAMA HAPA INAVYOELEZA:
Kwa kuwa shirika letu la SAWAKA limepokea malalamiko toka kwa wazee
katika sehemu mabalimbali za wilaya ya Karagwe na Kyerwa, wakilalamikia kuwa
wamerubuniwa na baadhi ya watu toka shirika lisilojulikana ambalo limeanza hivi
karibuni kwa kuwatoza wazee shs 2,500/= kwa kuwapatia vitambulisho vya kuwatambulisha
wazee kwa ajili ya matibabu na huduma mbalimbali bure toka serikalini na
kwamaba wazee hawa wamekuwa wakivipeleka vitambulisho hivyo katika vituo vya
Afya na Hospitali kama vile Hospital Teule Nyakahanga na kufukuzwa kwani havina uhalali
na havikutolewa na mamlaka husika.
Na wahusika wanaotoa vitambulisho hivi wamesikika katika
vyombo vya habari hapa Karagwe na Kyerwa wakizidi kuhamasisha wazee kununua
vitambulisho hivi vinavyolalamikiwa.
Hivyo, Tunatoa tamko Rasmi kwamba:
-Vitambulisho vya wazee vinavyotolewa na shirika hilo havina
uhalali wowote kwani havina baraka za serikali na havitambuliwi na mamlaka
husika na havina anuani wala muhuri wa wahusika kuthibitisha uhalali wake.
-SAWAKA Inatamka leo kwamba haina uhusiano wala ushirikiano
wowote na kundi hilo au shirika husika. Lakini tumefuatilia kwa makini sana na
kugundua kuwa hakuna shirika au Asasi iliyo hai ijulikanayo kama῝wazee wa Taifa la Tanzania῞ ambayo
imepewa jukumu la kutoa vitambulisho hapa nchini kama lipo ndio zile Asasi za
mfukoni ambazo zinatia doa shughuli za kazi nzuri za NGO’s.
-Wazee wanatahadharishwa kutochukua vitambulisho hivyo kwani
vinatia mashaka sana na kwamaba tunawataka viongozi wa matawi ya SAWAKA
yaliyopo huko vijijini kuwaelimisha wazee kuwa na subira ya kupata vitambulisho
vya mapema mwaka huu kama serikali ilivyokwisha toa ahadi.
- Vitambulisho hivi bandia kwa wazee vimeanza kutolewa
katika wilaya za Karagwe hasa Nyakahanga, Kihanga, Chanika, Nyaishozi, na
Ihembe, kuna uwezekano wa kundi hili kuendeleza mchezo huu katika wilaya zetu
jirani kama Muleba, Misenyi na Bukoba. Tunaomba washirika wetu tunaofanya nao
kazi kama TUWAMI, NA KWA WAZEE kuwahabarisha wazee kuhusu utapeli huu ambao
unaonekana kuwa mradi wa watu wachache wanaotafuta kujinufaisha na hela za
wazee.
-Hivyo, SAWAKA kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya
Karagwe na Kyerwa, itawajulisha utaratibu utakaotumika pindi serikali
ikikamilisha mchakato.
-Kutokana na tukio hili tumepeleka suala hili serikalini na
kuthibitisha kuwa vitambulisho hivi bandia na kutoa taarifa kwa vyombo husika
ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua husika{sheria}.
-Hivyo, tunaomba wazee kutoa ushirikiano wa kuwabaini
wanaotoa vitambulisho hivi kwa wazee.
Ahsante.
Tamko hili limetolewa na kusainiwa na
Mzee Nekemia Kazimoto
Mwenyekiti wa saidia wazee Karagwe SAWAKA .
Kwa vyombo vya habari.
No comments:
Post a Comment