Wednesday, June 19, 2013

HATUWEZI KUENDELEA KWA MTINDO HUU.




 HAWA NI WATOTO WA AFRICA, WANAFANYIWA UNYAMA NA UKATILI WA NAMNA HII.


Mtoto mchanga aliyekadiliwa kuwa na miezi mitano  amekutwa  metupwa katikati ya Barabara  katika  kitongoji cha kinoni kijiji Nyabwegira  kata ya ndama Wilayni karagwe.

Kichanga hicho ambacho kimekutwa kimekufa,  kwa mujibu wa mashuhuda wameeleza kuwa  kilionekana majira ya asubuhi ya jumapili 16june mwaka huu.

Jeshi la polisi wilayani karagwe  wakiongozwa na OCS Edward Masunga  pamoja na mganaga kutoka kituo cha Afya kayanga  John Makonga  wamefika eneo la tukio ambapo baada ya uchunguzi na taratibu zote kufanyika wameamuru mwili wa mtoto huyo kuzizwa eneo hilo.

Hata hivyo mganga makonga akiwa eneo la tukio baada ya uchunguzi na kuhojiwa na vyombo vya habari kama mimba imetolewa amesema kuwa imetoka bahati mbaya na kuwa kichanga hicho kilikuwa jinsia ya kike.

Pamoja na kuwa mwili wa mtoto huyo ulikutwa  hatua chache  karibu na makazi ya watu  lakini wananchi walizungumza na waandishi wa habari wamesema kuwa hakuna mtu katika kitongoji na kijiji hicho aliyekuwa na mimba.

Wananchi hao wameeleza kuwa  huenda aliyefanya kitendo hicho ametokea vijiji na vitongoji jirani.

Wamezungumzia  kitendo hicho kuwa cha  kinyama na kutaka vyombo vya dola kuchukua hatua kali kwa atakayebainika kuhusika na tukio hilo.

kwa upande wa Jeshi la polisi Wilayani Karagwe  wameomba wananchi pamoja na Vituo vya Afya ,zahanati na Hospitali Mkoanini Kagera kushirikiana na Jeshi hilo katika uchunguzi wa kumbaini aliyehusika na tukio hilo

Mpaka naripoti taarifa hii  hakuna aliyekamatwa kuhusika na tukio hilo.

Naye Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kagera Philip Karangi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba upelelezi unaendelea

No comments:

Post a Comment