Thursday, February 21, 2013

NI WATU WOTE WANAELEWA UMUHIMU WA REDIO.


Kwa utafiti uliofanywa na watafiti redio zimekuwa zikishika nafasi kubwa katika kuhabarisha, kuelimisha, kukosoa na kuburudisha.

Pamoja na kutambua umuhimu wake pia vyombo hivyo vya redio vinakumbana na changamoto kubwa ya watumiaji wa redio kwa upande mwingine tunaweza kuwaita walaji, kuna misuguano isiyokuwa na msingi, ushirikiano hafifu pia kutotambulika.

Sheria za vyombo vya habari vya redio zipo lakini katika usimamizi wake zinaelekea kama kuvibana na kutotoa nafasi kwa vyombo hivyo.

Hakuna sababu ya msingi inayoeleza bayana kwa nini chombo cha habari hasa redio kichukiwe, na utafiti wa kina wanaochukia vyombo vya habari wanakuwa wa namna gani na kwa nini?

Uhuru, uwazi na usawa ni vitu muhimu vya kuzingatia.






Wednesday, February 6, 2013

UUNGWANA.

 MAANA HALISI YA UUNGWANA.

Neno uungwana lina upana wake, shangaa watu wengi wamekuwa wepesi wa kutumianeno hili hata pasipostahili kwa uelewa wangu mdogo.

Aliyeua, aliyebaka, mkatili na muharibifu wa mali za watu ikifika wakati anaitwa muungwana anakumbatiwa na kuonekana wa maana mbele ya umma. je Uungwana ni nini maana yake?

Monday, January 28, 2013

KILIO CHA MLEMAVU BI MEDULED YOHANA KIMEPOKELEWA NA SHIRIKA LA WOMEDA.



        Bi meduled Yohana baada ya kutoa kilio chake kupitia vyombo vya habari shirika     lisilokuwa  la kiserikali WOMEDA Karagwe limejitokeza kumsaidia.


Bi Meduled Yohana ni mlemavu wa miguu yote miwili na  Anakabiliwa na chanamoto ya kutunza na kusomesha familia ya watoto {8} yatima wakati huo hakiwa hana mtaji na vifaa vya kuendesha shughuli zake za ushonaji wa chelehani akitumia mikono.
Cahangamoto nyingine ni malazi na chakula.